Ripoti ya Amnesty International toleo la mwaka 2025, Hali ya Haki za Binadamu Duniani, inatathmini maendeleo katika nyanja mbalimbali za haki za binadamu. Inabaini mienendo inayohusiana na ukiukwaji katika mapigano ya kivita, ukandamizaji wa upinzani, ubaguzi, udhalimu wa kiuchumi na wa tabianchi, na matumizi mabaya ya teknolojia ili kukiuka haki za binadamu. Pia inaangazia jinsi mataifa yenye nguvu yanavyodhooûsha kwa makusudi mfumo wa sheria, na hivyo kuzuia kutatuliwa kwa matatizo yanayoathiri maisha ya mamilioni ya watu.
Index Number: POL 10/8515/2025

