Toleo la mwaka 2026 la ripoti ya kila mwaka ya Amnesty International, Hali ya Haki za Binadamu Duniani, linatoa tathmini ya matukio kitaifa, kikanda na kimataifa kuhusu nyanja pana ya dhana za haki za binadamu. Linaangazia namna ambavyo nchi zilidhoofisha mfumo wa kimataifa wa kuzingatia kanuni, na kukwamisha utatuzi wa matatizo yanayoathiri maisha ya mamilioni. Pia linabainisha mienendo ya migogoro ya kivita, ukandamizaji wa maoni pinzani, ubaguzi, ukosekanaji wa haki ya kiuchumi na hali ya hewa, usitishaji wa ghafla wa misaada ya kibinadamu, na matumizi mabaya ya teknolojia. Ripoti hii inaelezea wasiwasi kuhusu haki za binadamu kwa mwaka 2025 kwa kuunganisha matukio ya kitaifa na kikanda na kuangalia mustakabali wa siku zijazo.
Index Number: POL 10/0320/2026

