Miaka 20 ya itifaki ya Maputo: azimio lisilofifia – kuendeleza na kulinda haki za wanawake na wasichana barani Afrika

Tunapoadhimisha miaka 20 tangu kuidhinishwa kwa Itifaki ya Mkataba wa Afrika kuhusu Haki za Binadamu na Watu kuhusiana na Haki za Wanawake barani Afrika (Itifaki ya Maputo), sisi, mashirika yaliyosaini hapa chini, tunapongeza mafanikio haya ya kuendeleza haki za wanawake na wasichana katika bara hili. Hati hii ya kisheria imeanzisha mfumo kamili unaoainisha viwango ambavyo nchi zinapaswa kuvifuata katika kuendeleza na kulinda haki za wanawake.

Choose a language to view report

Download PDF