Tanzania: Mwenyekiti wa chama cha upinzani lazima aachiwe huru: Tundu Lissu

Mnamo 9 Aprili, jeshi la polisi la Tanzania lilimtia nguvuni Tundu Lissu, Mwenyekiti wa chama kikuu cha upinzani nchini, Chadema (Chama cha Demokrasia na Maendeleo) baada ya kufanya mkutano wa hadhara Mbinga mjini, kusini magharibi mwa Tanzania. Baada ya hapo alihamishiwa Dar es Salaam, zaidi ya kilomita 1,000 kwa njia ya barabara wakati wa usiku. Polisi walitumia nguvu kupita kiasi, ikiwemo kurusha mabomu ya machozi na kupiga risasi hewani ili kuwatawanya wafuasi wake waliokuwa wamemzunguka wakati wa kutiwa nguvuni.

Choose a language to view report

Download PDF