Tanzania : Mkosoaji wa serikali hajulikani mahali alipo : Humphrey Polepole

Humphrey Polepole alitekwa jijini Dar es Salaam tarehe 6 Oktoba 2025 na askari wa usalama wasiojulikana. Ni mkosoaji mkubwa wa serikali ambaye amemkosoa Rais Samia Suluhu Hassan na chama tawala Chama Cha Mapinduzi (CCM) kwa uminyaji wa uhuru wa kiraia, ukandamizaji wa haki za binadamu na ushambuliaji wa wapinzani ikiwemo kufungwa kwa mwanasiasa wa upinzani Tundu Lissu. Serikali ya Tanzania lazima itaje mara moja hatima yake na mahali alipo, na kama yupo mikononi mwao, aachiwe mara moja.

Choose a language to view report

Download PDF