Kwa kutumia utafiti, uchambuzi wa mitandao ya kijamii na mahojiano na vijana Watetezi wa Haki za Binadamu, ripoti inaonyesha jinsi vurugu za mtandaoni na za maisha halisi zinavyohusishwa na madhara yanayowakumba vijana hawa na harakati za haki za binadamu kwa ujumla. Ripoti inatoa mwito kwa serikali ya Kenya kusitisha haraka vurugu za kiteknolojia dhidi ya waandamanaji wa amani na mashirika ya kiraia, na kuhakikisha wahanga wa matumizi mabaya ya nguvu wanapata haki na msaada.

