Tanzania: Matumizi ya sheria kama silaha: Ukandamizaji wa kisheria kabla ya Uchaguzi Mkuu Tanzania

Tanzania itafanya uchaguzi mkuu wake wa sita mnamo Oktoba 28, 2020 huku Rais John Pombe Magufuli akisaka kipindi cha pili cha miaka mitano. Uchaguzi huu unakuja huku kukiwa na kampeni ya ukandamizaji unaofanywa na serikali iliyoko madarakani kwa awamu yake ya kwanza ikilenga watu binafsi na mashirika yanayoikosoa serikali. Katika ripoti hii, tunaangazia hali ya kutisha ya haki za binadamu katika kipindi cha kuelekea uchaguzi na tunatoa wito kwa serikali ya Tanzania kuheshimu na kulinda haki za binadamu katika kipindi chote cha uchaguzi na baada ya hapo.

Choose a language to view report

Download PDF