Hukumu za kifo na watu walionyongwa 2022

Utafiti wa Amnesty International kuhusu matumizi ya adhabu ya kifo mwaka wa 2022 ulionyesha kwamba kulikuwa na ongezeko kubwa la idadi ya watu wanaojulikana kuwa walinyongwa duniani, likiwemo ongezeko kubwa la watu walionyongwa kutokana na makosa yanayohusiana na dawa za kulevya. Mwenendo huu mbaya unakinzana na mwenendo mwingine mzuri tunaouona kwa sasa: yaani, nchi kadhaa zilichukua hatua kuondokana na adhabu ya kifo mwaka wa 2022, huu ukiwa ufanisi mkubwa katika kumaliza adhabu iliyo katili, yenye kukosa ubinadamu na ya kushusha hadhi ya binadamu kuliko adhabu nyngine yoyote.

Choose a language to view report

Download PDF